Psalms 31:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimekuwa dharau kwa maadui zangu wote; kioja kwa majirani zangu. Rafiki zangu waniona kuwa kitisho; wanionapo njiani hunikimbia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na majirani zangu, hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, wale wanaoniona barabarani wananikimbia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimekuwa dharau kwa maadui zangu wote; kioja kwa majirani zangu. Rafiki zangu waniona kuwa kitisho; wanionapo njiani hunikimbia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na jirani zangu, hata rafiki zangu wananiogopa, wale wanionao barabarani hunikimbia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na jirani zangu, hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, wale wanionao barabarani hunikimbia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu ya watesi wangu nimelaumiwa, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Wanaoniona njiani wananikimbia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimekuwa dharau kwa maadui zangu wote; kioja kwa majirani zangu. Rafiki zangu waniona kuwa kitisho; wanionapo njiani hunikimbia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawa wa kufyozwa tu kwao wanisongao, hata kwa wenzangu wa kukaa nao ni vivyo hivyo, nao rafiki zangu ninawatia woga, wanionao njiani hunikimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maisha yangu yamekwisha kwa ajili ya kuugua; nayo miaka yangu kwa ajili ya kusikitika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka.