Psalms 31:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nasikia watu wakinongonezana, vitisho kila upande; wanakula njama dhidi yangu, wanafanya mipango ya kuniua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nasikia watu wakinong'onezana, vitisho kila upande; wanakula njama dhidi yangu, wanafanya mipango ya kuniua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na watu wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri ya pamoja dhidi yangu na kula njama kuniua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nimesikia wengi wakinong'onezana; Hofu katika pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walipanga kunitoa uhai wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nasikia watu wakinongonezana, vitisho kila upande; wanakula njama dhidi yangu, wanafanya mipango ya kuniua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikasikia wengi, wakinong'onezana: Pande zote pia anastukwia tu; wakanilia njama wote pamoja, wakawaza, ndivyo waone njia ya kunitoa roho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nimesikia masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimesahaulika kama mutu aliyekufa; nimekuwa kama chungu kilichovunjikavunjika.