Psalms 31:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami niliogopa na kudhani kwamba ulikuwa umenitupa; kumbe, ulisikia kilio changu nilipokuita unisaidie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nalisema kwa haraka yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya dua yangu Wakati nilipokulilia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami niliogopa na kudhani kwamba ulikuwa umenitupa; kumbe, ulisikia kilio changu nilipokuita unisaidie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa haraka yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami niliogopa na kudhani kwamba ulikuwa umenitupa; kumbe, ulisikia kilio changu nilipokuita unisaidie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami kwa woga wangu nilikua nimesema: Nimetupwa, niondoke penye macho yako, yasinione tena. Lakini malalamiko yangu umeyasikia kweli hapo, nilipokulilia, unisaidie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nalisema kwa haraka yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya dua yangu Wakati nilipokulilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe asifiwe, maana amenionyesha wema wake wa ajabu, nilipozungukwa katika muji unaoshambuliwa.