Psalms 35:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote: “Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe! Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu, maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitapaza sauti yangu nikisema, “Ni nani aliye kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu? Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale waliowazidi nguvu, unawaokoa maskini na wahitaji kutokana na wanaowanyang’anya!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mifupa yangu yote itasema, Bwana, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote: “Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe! Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu, maskini na fukara mikononi mwa wanyang'anyi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitapaza sauti yangu nikisema, “Ni nani aliye kama wewe, Ee BWANA? Huwaokoa maskini kutokana na watu walio na nguvu kuliko wao, maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyang'anya!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitapaza sauti yangu nikisema, “Ni nani aliye kama wewe, Ee bwana? Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao, maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyang’anya!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mifupa yangu yote itasema, BWANA, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini kutoka kwa mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote: “Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe! Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu, maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, itakaposema nayo mifupa yangu yote: Bwana, afananaye nawe yuko wapi? Unamponya mnyonge mkononi mwake yeye ampitaye nguvu, kweli huponya mnyonge na mkiwa mikononi mwao wamnyang'anyao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mifupa yangu yote itasema, BWANA, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitamwambia Yawe kwa moyo wangu wote: “Wewe, ee Yawe, hakuna anayekuwa kama wewe! Wewe unawaokoa wamasikini kutoka makucha ya wenye nguvu, wamasikini na wakosefu kutoka mikono ya wanyanganyi.”