Psalms 35:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “Mwenyezi Mungu atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe Bwana, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki na wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “BWANA atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “ bwana atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wao waliopendezwa na wongofu wangu sharti wapige vigelegele kwa kufurahiwa! Sharti waseme pasipo kukoma: Mkuu ni Bwana, mtumishi wake akikaa na kutengemana, hupendezwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wanaotaka kuona kwamba sina kosa, wakuwe na furaha tele, waseme siku zote: “Yawe ni mukubwa! Anapendezwa na kumupatia mutumishi wake uheri.”