Psalms 38:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nakuomba tu maadui wasinisimange, wasione fahari juu ya kuanguka kwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wajitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakuomba tu maadui wasinisimange, wasione fahari juu ya kuanguka kwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakuomba tu maadui wasinisimange, wasione fahari juu ya kuanguka kwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nimesema: hawatafurahi kamwe na kunicheka; kama mguu wangu ungejikwaa, wangejivuna na kunibeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninakutumainia wewe, ee Yawe; wewe, ee Yawe, Mungu wangu, ndiwe utakayenijibu.