Psalms 39:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi) Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Yeduthuni. Zaburi Ya Daudi) Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilisema: Nitaziangalia njia zangu, nisiukoseshe ulimi wangu; nacho kinywa changu nitakiangalia na kukifumba, asiyemcha Mungu akingali yuko mbele yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa Yedutuni. Zaburi ya Daudi.