Psalms 39:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee Mwenyezi Mungu, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, mhamiaji, kama walivyokuwa baba zangu wote,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee BWANA, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee bwana, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu; usikilize kilio changu, usikae kimya ninapolia. Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye, ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana, yasikie maombo yangu! Vilio vyangu sharti vifike masikioni mwako! Nayo machozi yangu usiyanyamazie! Kwani mimi ni mgeni tu apangaye kwako, kama baba zangu wote walivyokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unapomwazibu mutu zambi zake kwa kumwadibisha, unaharibu kama nondo kile anachokipenda. Hakika, kila mwanadamu ni kama pumzi tu!