Psalms 39:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbe umenipimia maisha mafupi sana! Maisha yangu si kitu mbele yako. Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umefanya maisha yangu mafupi kama nyanda; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbe umenipimia maisha mafupi sana! Maisha yangu si kitu mbele yako. Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbe umenipimia maisha mafupi sana! Maisha yangu si kitu mbele yako. Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, siku zangu, ulizonipa, ni zenye upana kama wa kiganja tu; mbele yako nipo kama mtu asiyekuwapo. Kweli kila mtu, ijapo awe mwenye nguvu, ni mvuke tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ee Yawe, unijulishe mwisho wangu, siku zangu za kuishi zimenibakia ngapi, nijue namna maisha yangu yanavyopita upesi!”