Psalms 40:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maafa yasiyohesabika yanizunguka, maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona; ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu, nami nimevunjika moyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana taabu zisizohesabika zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Na moyo wangu umeniacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maafa yasiyohesabika yanizunguka, maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona; ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu, nami nimevunjika moyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Nami nimevunjika moyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maafa yasiyohesabika yanizunguka, maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona; ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu, nami nimevunjika moyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani makosa yasiyohesabika yalinizunguka, manza, nilizozikora, zikanirudia, nisiweze kuziona zote, ni nyingi sana kuliko nywele za kichwani pangu; ndipo, moyo wangu ulipojiendea, ukanipotelea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Na moyo wangu umeniacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, usikose kunirehemu! Wema na uaminifu wako vinilinde.