Psalms 40:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanaonuia kuniangamiza, na waaibike na kufedheheka! Hao wanaotamani niumie, na warudi nyuma na kuaibika!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wote wanaotafuta kuniua, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, wafukuzwe mbali kwa aibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waaibike, wafedheheke pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanaonuia kuniangamiza, na waaibike na kufedheheka! Hao wanaotamani niumie, na warudi nyuma na kuaibika!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu na waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu na warudishwe nyuma kwa aibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waaibike na wafedheheke, Wote wanaotaka kuniua. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanaonuia kuniangamiza, na waaibike na kufedheheka! Hao wanaotamani niumie, na warudi nyuma na kuaibika!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti wapatwe na soni kwa kutwezwa wao wote pamoja walioitafuta roho yangu, waiangamize! Sharti warudishwe nyuma, nyuso ziwaive kwa soni waliopendezwa na mabaya yaliyonipata mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waaibike, wafedheheke pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upendezwe, ee Yawe, kuniokoa; ee Yawe, ukuje haraka kunisaidia.