Psalms 40:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wote wale wanaokutafuta wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wote wanaokutafuta washangilie na kukufurahia, wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, “Mwenyezi Mungu atukuzwe!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wote wale wanaokutafuta wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bali wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “BWANA atukuzwe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “ bwana atukuzwe!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Washangilie na wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, BWANA ni Mkuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wote wale wanaokutafuta wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti wachangamke na kufurahiwa wote wakutafutao! Waupendao wokovu wako waseme pasipo kukoma: Mkuu ni Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao wanaonisimanga, wafezeheke kwa kushindwa kwao!