Psalms 40:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu; mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno, watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Heri mtu yule amfanyaye Mwenyezi Mungu kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu; mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno, watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Heri mtu yule amfanyaye BWANA kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Heri mtu yule amfanyaye bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu; mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno, watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye shangwe ni mtu amtumiaye Bwana kuwa egemeo lake, asiyewageukia wajivunao, wala wao wanaodanganya na kutumikia uwongo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alinifundisha wimbo mupya, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona, wataogopa, na kisha watamutumainia Yawe.