Psalms 40:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe hutaki tambiko wala sadaka, tambiko za kuteketeza wala za kuondoa dhambi; lakini umenipa masikio nikusikie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe hutaki tambiko wala sadaka, tambiko za kuteketeza wala za kuondoa dhambi; lakini umenipa masikio nikusikie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu, sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Umeyazibua masikio yangu; Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe hutaki tambiko wala sadaka, tambiko za kuteketeza wala za kuondoa dhambi; lakini umenipa masikio nikusikie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ng'ombe na vyakula vya tambiko hakupendezwa navyo, lakini umenizibua masikio yangu; ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa nzima navyo vipaji vya tambiko vya kulipa makosa hukuvitaka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, Mungu wangu, umetufanyia maajabu mengi, na mipango yako juu yetu haihesabiki; hakuna yeyote anayekuwa kama wewe. Kama ningeweza kusimulia hayo yote, hesabu yake ingenishinda.