Psalms 42:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu: Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu, nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani; umati wa watu wakifanya sherehe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati wa watu waliosherehekea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu: jinsi nilivyokwenda na umati wa watu, nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani; umati wa watu wakifanya sherehe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vitu hivi ninavikumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati wa watu wanaoadhimisha sikukuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati uliosherehekea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu: Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu, nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani; umati wa watu wakifanya sherehe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, ninapoumimina moyo wangu ndani yangu kwa kuvikumbuka hivyo, nilivyokwenda na kikosi cha watu nilipowaongoza na kuwapeleka Nyumbani kwa Mungu, wao wakipiga vigelegele vya kumshukuru, wakawa kundi kubwa la watu waliokula sikukuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Machozi ni chakula changu muchana na usiku; ninaambiwa kila siku: “Mungu wako yuko wapi?”