Psalms 44:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wako hawakuitwaa nchi kwa silaha zao, wala hawakupata ushindi kwa nguvu zao; ila uliwasalimisha kwa mkono wako mwenyewe, kwa kuwaangazia uso wako, kwani wewe uliwapenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi, Wala si mkono wao uliowaokoa; Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wako hawakuitwaa nchi kwa silaha zao, wala hawakupata ushindi kwa nguvu zao; ila uliwasalimisha kwa mkono wako mwenyewe, kwa kuwaangazia uso wako, kwani wewe uliwapenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wako hawakuitwaa nchi kwa silaha zao, wala hawakupata ushindi kwa nguvu zao; ila uliwasalimisha kwa mkono wako mwenyewe, kwa kuwaangazia uso wako, kwani wewe uliwapenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nchi hawakuitwaa kwa nguvu za panga zao, wala mikono yao siyo iliyowashindisha, ila mkono wako wa kuume na mwanga wa uso wako ndio uliovifanya kwa kupendezwa nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi, Wala si mkono wao uliowaokoa; Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mukono wako mwenyewe uliyafukuza mataifa, na mahali pao ukawaikalisha watu wako; uliyaazibu mataifa, na kuwafanikisha watu wako.