Psalms 45:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yungiyungi. Utenzi wa Wakorahi; utenzi wa mapenzi) Moyo wangu umejaa mawazo mema: Namtungia mfalme shairi langu, ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Moyo wangu umejaa mawazo mema: namtungia mfalme shairi langu, ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Wana Wa Kora) Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu, ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Moyo wangu umejaa mawazo mema: Namtungia mfalme shairi langu, ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Moyo wangu umefurika, utunge maneno mema; kwa kumfanyizia mfalme kazi mimi ninayesema. Ulimi wangu ni kalamu ya fundi ajuaye kuandika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo: “Mayungiyungi.” Mashairi ya Wakora. Wimbo wa mapenzi.