Psalms 49:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wataongozwa kama kondoo hadi kuzimu, kifo kitakuwa mchungaji wao. Watashuka moja kwa moja kaburini. Miili yao itaozea huko, Kuzimu kutakuwa makao yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wataongozwa kama kondoo hadi kuzimu, kifo kitakuwa mchungaji wao. Watashuka moja kwa moja kaburini. Miili yao itaozea huko, Kuzimu kutakuwa makao yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama kondoo wamewekewa kwenda kaburini na kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wataongozwa kama kondoo hadi kuzimu, kifo kitakuwa mchungaji wao. Watashuka moja kwa moja kaburini. Miili yao itaozea huko, Kuzimu kutakuwa makao yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama kondoo wanashurutizwa kwenda kuzimuni, mwenye kuwachunga ndiye kifo. Wanyokao mioyo watawatawala hapo patakapokucha; ndipo, ubishi wao utakapoishia, watakapokaa kuzimuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hayo ndiyo yanayowapata wanaojitumainia kwa upumbafu, ndio mwisho wa wale wanaojivunia mali zao.