Psalms 50:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu wetu anakuja, na sio kimyakimya: Moto uunguzao wamtangulia, na dhoruba kali yamzunguka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu wetu anakuja, na sio kimyakimya: moto uunguzao wamtangulia, na dhoruba kali yamzunguka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu wetu atakuja wala sio kimya kimya, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu wetu anakuja, na sio kimyakimya: Moto uunguzao wamtangulia, na dhoruba kali yamzunguka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu wetu anakuja, hanyamazi; moto ulao unamtangulia, upepo uvumao na nguvu unamzinga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu wetu anakuja, lakini si kimyakimya: moto wenye kuteketeza unamutangulia, na zoruba kali inamuzunguka.