Psalms 52:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tazameni yaliyompata mtu huyu! Yeye hakutaka Mungu awe kimbilio lake; bali alitegemea wingi wa mali yake, na kutafuta humo usalama wake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tazameni yaliyompata mtu huyu! Yeye hakutaka Mungu awe kimbilio lake; bali alitegemea wingi wa mali yake, na kutafuta humo usalama wake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tazameni yaliyompata mtu huyu! Yeye hakutaka Mungu awe kimbilio lake; bali alitegemea wingi wa mali yake, na kutafuta humo usalama wake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Mungu naye atakuponda, akutoweshe kale na kale, kwenye kituo chako atakupokonya, akung'oe katika nchi yao walio hai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Mungu atakuangamiza milele, atakunyanyua na kukuondoa katika nyumba yako; atakuongoa katika inchi ya wenye kuishi.