Psalms 55:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maneno yake ni laini kuliko siagi, lakini mawazo yake ni ya kufanya vita. Maneno yake ni mororo kama mafuta, lakini yanakata kama upanga mkali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Bali hayo ni panga wazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maneno yake ni laini kuliko siagi, lakini mawazo yake ni ya kufanya vita. Maneno yake ni mororo kama mafuta, lakini yanakata kama upanga mkali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake, maneno yake mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maneno yake ni laini kuliko siagi, lakini mawazo yake ni ya kufanya vita. Maneno yake ni mororo kama mafuta, lakini yanakata kama upanga mkali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana wanawakamata nao waliomkalia Mungu, nalo Agano lake wanalipinga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Bali hayo ni panga wazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwenzangu amemushambulia rafiki yake, amevunja mapatano yake.