Psalms 55:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtwike BWANA fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtwike bwana fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wayasemayo ni mafuta ya midomo, ni matamu kuliko maziwa, lakini mioyoni mwao huwaza vita. Maneno yao, wayasemayo, hulegea kuliko mafuta ya uto, lakini wenyewe ndio panga zilizokwisha kuchomolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maneno yake ni matamu kuliko maziwa, lakini mawazo yake ni ya kufanya vita. Maneno yake ni laini kama mafuta, lakini yanakata kama upanga mukali.