Psalms 55:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe, ee Mungu, utawaporomosha shimoni chini kabisa, watu hao wauaji na wadanganyifu; hao hawatafikia nusu ya maisha yao. Lakini mimi nitakutumainia wewe ee Mungu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi ninakutumaini wewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe, Ee Mungu, utawatelemsha, Walifikilie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe, ee Mungu, utawaporomosha shimoni chini kabisa, watu hao wauaji na wadanganyifu; hao hawatafikia nusu ya maisha yao. Lakini mimi nitakutumainia wewe ee Mungu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi, ninakutumaini wewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi ninakutumaini wewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe, ee Mungu, utawaporomosha shimoni chini kabisa, watu hao wauaji na wadanganyifu; hao hawatafikia nusu ya maisha yao. Lakini mimi nitakutumainia wewe ee Mungu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umtupie bwana yakulemeayo! Yeye atakumalizia, hatamtoa mwongofu, atikisike kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe, Ee Mungu, utawatelemsha, Walifikilie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utue muzigo wako kwa Yawe, naye atakusaidia; hamwachilii mutu wa haki ashindwe.