Psalms 57:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi alipomponyoka Shauli na kujificha pangoni) Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana kwako nakimbilia usalama. Kivulini mwa mabawa yako nitakimbilia usalama, hata hapo dhoruba ya maangamizi itakapopita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mabawa yako nitakimbilia hadi maafa yapite.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana kwako nakimbilia usalama. Kivulini mwa mabawa yako nitakimbilia usalama, hata hapo dhoruba ya maangamizi itakapopita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Usiharibu! Utenzi Wa Daudi Baada Ya Kumponyoka Sauli Pangoni) Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana kwako nakimbilia usalama. Kivulini mwa mabawa yako nitakimbilia usalama, hata hapo dhoruba ya maangamizi itakapopita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nihurumie, Mungu! Nihurumie! Kwani roho yangu imekukimbilia wewe, kivuli kilichoko mabawani kwako nimekikimbilia, mpaka yaishe kupita mateso haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Usiharibu.” Mashairi ya Daudi alipomuponyoka Saulo na kujificha katika pango.