Psalms 59:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu Mwenye Nguvu, Mungu wa Israeli. Uamke, uwaadhibu hao watu wasiokujua; usiwaache hao wanaopanga ubaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mungu, Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, uliye Mungu wa Israeli, zinduka uyaadhibu mataifa yote; usioneshe huruma kwa wasaliti waovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Wewe, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uamke. Uwapatilize mataifa yote; Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu Mwenye Nguvu, Mungu wa Israeli. Uamke, uwaadhibu hao watu wasiokujua; usiwaache hao wanaopanga ubaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! Zinduka uyaadhibu mataifa yote, usionyeshe huruma kwa wasaliti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! Zinduka uyaadhibu mataifa yote, usionyeshe huruma kwa wasaliti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uinuke. Uwapatilize mataifa yote; Usimrehemu hata mmoja wa wale wapangao maovu kwa hila.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu Mwenye Nguvu, Mungu wa Israeli. Uamke, uwaadhibu hao watu wasiokujua; usiwaache hao wanaopanga ubaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe Bwana Mungu, uliye Mwenye vikosi, uliye Mungu wa Isiraeli, inuka, uwapatilize wamizimu wote! Usiwahurumie hata mmoja wao waliokuacha kwa upotovu tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uamke. Uwapatilize mataifa yote; Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa sina kosa, wanakimbia, ee Yawe, kujiweka tayari. Uinuke, ee Yawe, uwaangalie na kunisaidia!