Psalms 63:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hao wanaotaka kuyaangamiza maisha yangu, watatumbukia chini kwenye makao ya wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaotafuta uhai wangu wataangamizwa; wataenda chini kwenye vilindi vya dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, Wataingia pande za nchi zilizo chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hao wanaotaka kuyaangamiza maisha yangu, watatumbukia chini kwenye makao ya wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa, watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa, watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiangamiza, Wataingia katika vilindi vya nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hao wanaotaka kuyaangamiza maisha yangu, watatumbukia chini kwenye makao ya wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wao wanaoitafuta roho yangu, waiangamize, sharti washuke kuzimuni huko ndani ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu, Wataingia pande za nchi zilizo chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Roho yangu inashikamana nawe kabisa; unanilinda kwa mukono wako wa kuume.