Psalms 64:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu, wanamshambulia ghafla bila kuogopa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hurusha mishale kutoka mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu, wanamshambulia ghafla bila kuogopa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hutupa mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafla humpiga bila kuogopa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toka mafichoni wamshambulia mtu mnyofu, wanamshambulia ghafla bila kuogopa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndimi zao wamezinoa, ziwe zenye ukali kama wa upanga, mishale yao, wanayotaka kuipiga, ni maneno machungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wananoa ndimi zao kama upanga, nayo maneno yao ni makali kama mishale.