Psalms 68:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake; mtengenezeeni njia yake apandaye mawinguni. Jina lake ni Mwenyezi-Mungu; furahini mbele yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mtukuzeni yeye anayepita juu ya mawingu: jina lake ni Mwenyezi Mungu, furahini mbele zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake; mtengenezeeni njia yake apandaye mawinguni. Jina lake ni Mwenyezi-Mungu; furahini mbele yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mwinueni juu yeye aendeshwaye juu ya mawingu, jina lake ni BWANA, furahini mbele zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu: jina lake ni bwana, furahini mbele zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mwimbieni wimbo yeye apitaye katika mawingu, Jina lake ni YAHU; Shangilieni mbele zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake; mtengenezeeni njia yake apandaye mawinguni. Jina lake ni Mwenyezi-Mungu; furahini mbele yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwimbieni Mungu, nalo Jina lake lishangilieni! Mtengenezeeni njia apitaye nyikani! Bwana ni Jina lake, mpigieni vigelegele!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wa haki wanafurahi Mungu anapokuja, wanashangilia na kuimba kwa furaha.