Psalms 69:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengi kuliko nywele zangu ndio wanichukiao bure. Wana nguvu sana hao wanaotaka kuniua, hao wanaonishambulia kwa mambo ya uongo. Je, nirudishe kitu ambacho sikuiba?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengi kuliko nywele zangu ndio wanichukiao bure. Wana nguvu sana hao wanaotaka kuniua, hao wanaonishambulia kwa mambo ya uongo. Je, nirudishe kitu ambacho sikuiba?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengi kuliko nywele zangu ndio wanichukiao bure. Wana nguvu sana hao wanaotaka kuniua, hao wanaonishambulia kwa mambo ya uongo. Je, nirudishe kitu ambacho sikuiba?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikachoka kwa kupiga kelele, mmeo ukakauka, nikizidi kumtazamia Mungu wangu, macho yakanizimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaregea kwa ajili ya kulalamika, na koo langu limekauka. Macho yangu yamefifia, nikikungojea ewe Mungu wangu.