Psalms 7:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amka kwa hasira yako, Ee Mwenyezi Mungu, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana uondoke kwa hasira yako; Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amka kwa hasira yako, Ee BWANA, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Uamke, Mungu wangu, uamue haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amka kwa hasira yako, Ee bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inuka, Bwana, kwa makali yako! Jikweze, ukinge moto wa makorofi yao wanisongao! Amka, uje kwangu wewe uliyeagiza kuhukumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, adui anifuatilie na kunikamata, akomeshe maisha yangu na kuuzika uzima wangu ndani ya mavumbi.