Psalms 70:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wote wanaokutafuta washangilie na kukufurahia, wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, “Mwenyezi Mungu ni mkuu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wote wakutafutao na washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako daima na waseme, “Mungu na atukuzwe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wote wale wanaokutafuta, wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mungu ni mkuu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti wachangamke na kufurahiwa wote wakutafutao! Waupendao wokovu wako waseme pasipo kukoma: Mkuu ni Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wapumbazike kwa haya, hao wanaofurahia kunizomea!