Psalms 71:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uwe mwamba wangu wa kukimbilia usalama, ngome imara ya kuniokoa, kwani wewe ni mwamba na ngome yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda sikuzote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uwe mwamba wangu wa kukimbilia usalama, ngome imara ya kuniokoa, kwani wewe ni mwamba na ngome yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uwe mwamba wa kimbilio langu, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uwe mwamba wangu wa kukimbilia usalama, ngome imara ya kuniokoa, kwani wewe ni mwamba na ngome yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Niwie mwamba wenye nguvu, niujie siku zote, maana uliniagia, ya kuwa utaniokoa. Kwani mwamba wangu na boma langu ndiwe wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda sikuzote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukuwe kikingio changu cha kukimbilia, kimbilio lenye nguvu la kuniokoa, kwa maana wewe ni kikingio na kimbilio langu.