Psalms 72:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jina la mfalme litukuke daima; fahari yake idumu pindi liangazapo jua. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mbarikiwa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jina la mfalme litukuke daima; fahari yake idumu pindi liangazapo jua. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mbarikiwa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia yeye, nao watamwita mbarikiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jina la mfalme litukuke daima; fahari yake idumu pindi liangazapo jua. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mbarikiwa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jina lake na liwepo kale na kale! Siku zote, jua likingali liko, jina lake na lichipuke, watu wa mataifa yote wajibariki na kulitaja pamoja na kulishangilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jina lake na lidumu milele, Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jina la mufalme litukuzwe siku zote; utukufu wake udumu muda wote jua litakapokuwa. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mwenye heri!