Psalms 75:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, anashika kikombe mkononi, kimejaa divai kali ya hasira yake; anaimimina na waovu wote wanainywa; naam, wanainywa mpaka tone la mwisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkononi mwa Mwenyezi Mungu kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa hata tone la mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, anashika kikombe mkononi, kimejaa divai kali ya hasira yake; anaimimina na waovu wote wanainywa; naam, wanainywa mpaka tone la mwisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkononi mwa BWANA kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkononi mwa bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na hasira yake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, anashika kikombe mkononi, kimejaa divai kali ya hasira yake; anaimimina na waovu wote wanainywa; naam, wanainywa mpaka tone la mwisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Mungu ndiye anayeamua; yeye ndiye anayenyenyekeza, tena ndiye anayekweza.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu mwenyewe ndiye mwamuzi; anamushusha mumoja na kumwinua mwingine.