Psalms 79:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa nini mataifa yatuambie: “Yuko wapi Mungu wenu?” Utujalie tuone ukiwalipiza watu wa mataifa mauaji ya watumishi wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wenu?” Mbele ya macho yetu, dhihirisha kati ya mataifa kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa ya watumishi wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao? Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika Kijulike kati ya mataifa machoni petu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa nini mataifa yatuambie: “Yuko wapi Mungu wenu?” Utujalie tuone ukiwalipiza watu wa mataifa mauaji ya watumishi wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wenu?” Mbele ya macho yetu, dhihirisha kati ya mataifa kwamba unalipiza kisasi cha damu iliyomwagwa ya watumishi wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wenu?” Mbele ya macho yetu, dhihirisha kati ya mataifa kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa ya watumishi wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa nini mataifa yaseme, Yuko wapi Mungu wao? Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika Kijulikane kati ya mataifa machoni petu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa nini mataifa yatuambie: “Yuko wapi Mungu wenu?” Utujalie tuone ukiwalipiza watu wa mataifa mauaji ya watumishi wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mbona wamizimu waseme: Mungu wao yuko wapi? Sharti tuvione na macho yetu, vikitambulikana kwao wamizimu, jinsi unavyozilipiza damu zilizomwagwa za watumishi wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao? Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika Kijulike kati ya mataifa machoni petu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa nini mataifa yatuambie: “Mungu wenu yuko wapi?” Utujalie tuone jinsi utakavyowalipiza mataifa kisasi kwa ajili ya mauaji ya watumishi wako.