Psalms 84:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Gitithi. Zaburi ya Wakorahi) Jinsi gani yanavyopendeza makao yako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, makao yako yapendeza kama nini!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jinsi gani yanavyopendeza makao yako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Wana Wa Kora) Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maskani yako yapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jinsi gani yanavyopendeza makao yako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa mwimbishaji, wa kuimba kama wimbo wa wagemaji? Wimbo wa wana wa Kora.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maskani zako zapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mukubwa wa waimbaji: kwa mutindo wa watu wa Gati: Zaburi ya Wakora.