Psalms 84:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu ni jua na ngao; Mwenyezi Mungu hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa BWANA ni jua na ngao, BWANA hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa bwana ni jua na ngao, bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani siku moja ya kukaa katika nyua za Bwana ni nzuri kuliko nyingine, ijapo ziwe elfu. Kungoja zamu mlangoni kwa nyumba ya Mungu kwanipendeza kuliko kukaa mahemani kwao wasiomcha Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja tu ndani ya hekalu lako, ni bora kuliko siku elfu pahali pengine; afazali kubakia kwa mulango wa nyumba yako, kuliko kuishi ndani ya nyumba ya waovu.