Psalms 88:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimeteseka na kukaribia kifo tangu ujana wangu; nateseka kwa mapigo yako, niko hoi kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na mapigo yako, nami nimekata tamaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana, Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimeteseka na kukaribia kifo tangu ujana wangu; nateseka kwa mapigo yako, niko hoi kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tangu ujana wangu nimeteseka nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako nami nimekata tamaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimeteswa tangu ujana wangu na niko karibu kufa, Nimeumia kwa mapigo yako; nami nimekata tamaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimeteseka na kukaribia kifo tangu ujana wangu; nateseka kwa mapigo yako, niko hoi kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbona unaitupa roho yangu, wewe Bwana? Mbona unauficha uso wako, nisiuone?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana, Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbona, ee Yawe, unanitupilia mbali? Kwa nini unanificha uso wako?