Psalms 88:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ghadhabu yako imeniwakia; mashambulio yako ya kutisha yananiangamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghadhabu yako imepita juu yangu; mapigo yako yameniangamiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hasira zako kali zimepita juu yangu, Maogofyo yako yameniangamiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ghadhabu yako imeniwakia; mashambulio yako ya kutisha yananiangamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hasira zako kali zimenizidia, Mapigo yako yatishayo yameniangamiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ghadhabu yako imeniwakia; mashambulio yako ya kutisha yananiangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi ni mnyonge na mwele toka utoto wangu, nikayavumilia mastuko yako, kisha nikazimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hasira zako kali zimepita juu yangu, Maogofyo yako yameniangamiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimeteseka na kukaribia kifo tangu ujana wangu; ninateseka kwa mapigo yako, niko tabani kabisa.