Psalms 90:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu! Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu! Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, ikiwa tuna nguvu ni miaka themanini, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu! Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zetu za kuwapo ni miaka sabini, kama tunazidi kuwa wenye nguvu, ni miaka themanini. Nayo masumbuko na mateso ndio urembo wao; kwa kuwa tunaruka kama ndege, zinapita upesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muda wa maisha yetu ni miaka makumi saba, au tukikuwa wenye afya, miaka makumi nane; lakini yote ni shida na taabu! Siku zinapita mbio, nasi tunatoweka!