Psalms 93:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu anatawala; amejivika fahari kuu! Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu! Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu; Mwenyezi Mungu amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu anatawala; amejivika fahari kuu! Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu! Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA anatawala, amejivika utukufu; BWANA amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana anatawala, amejivika utukufu; bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu anatawala; amejivika fahari kuu! Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu! Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Bwana ni mfalme, huvaa yenye urembo; kweli Bwana huvaa, nayo nguvu ndiyo, aliyojifunga kiunoni. Hivyo ndivyo, alivyoishikiza nchi, isije kuyumbayumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anatawala; amejifunika utukufu mukubwa! Yawe amevaa utukufu na nguvu! Ameimarisha ulimwengu, hautatikisika hata kidogo.