Psalms 98:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu; imsifu kwa nyimbo na vigelegele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu; imsifu kwa nyimbo na vigelegele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpigieni kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpigieni bwana kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu; imsifu kwa nyimbo na vigelegele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpigieni Bwana shangwe, nchi zote! Pazeni sauti! Shangilieni na kumwimbia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Dunia yote imushangilie Yawe; imusifu kwa nyimbo na vigelegele.