Psalms 99:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose na Aroni walikuwa makuhani wake; Samueli alikuwa miongoni mwa waliomlilia. Walimlilia Mwenyezi-Mungu naye akawasikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Mwenyezi Mungu, naye aliwajibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose na Aroni walikuwa makuhani wake; Samueli alikuwa miongoni mwa waliomlilia. Walimlilia Mwenyezi-Mungu naye akawasikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita naye aliwajibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita bwana, naye aliwajibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose na Aroni walikuwa makuhani wake; Samueli alikuwa miongoni mwa waliomlilia. Walimlilia Mwenyezi-Mungu naye akawasikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose na Haroni walikuwa miongoni mwao watambikaji wake, Samueli alikuwa miongoni mwao waliolililia Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa na Haruni walikuwa makuhani wake; Samweli alikuwa kati ya waliomulilia. Walimulilia Yawe naye akawasikiliza.