Revelation 1:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na katikati yake kulikuwa na kitu kama Mwana wa Mtu, naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na mkanda wa dhahabu kifuani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na katikati ya vile vinara vya taa, alikuwamo mtu kama Mwana wa Adamu, akiwa amevaa joho refu, na mkanda wa dhahabu ukiwa umefungwa kifuani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikamwona mmoja katikati ya vinara aliyeonekana kama Mwana wa Mtu. Alikuwa amevaa vazi refu, na mshipi wa dhahabu uliofungwa kuzunguka kifua chake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na katikati yake kulikuwa na kitu kama mtu, naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na ukanda wa dhahabu kifuani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na katikati yake kulikuwa na kitu kama Mwana wa Mtu, naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na mkanda wa dhahabu kifuani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
katikati ya vile vinara vya taa, nikaona mtu kama Mwana wa Adamu, amevaa joho refu na mkanda wa dhahabu umefungwa kifuani mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na katikati ya vile vinara vya taa, alikuwamo mtu kama Mwana wa Adamu, akiwa amevaa joho refu, na mkanda wa dhahabu ukiwa umefungwa kifuani mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu kifuani
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na katikati yake kulikuwa na kitu kama Mwana wa Mtu, naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na mkanda wa dhahabu kifuani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katikati ya hizo taa nikaona mwenye kufanana na Mwana wa mtu. Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu, napo kifuani alikuwa amejifunga mkanda wa dhahabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na katikati ya vile vinara saba, nikaona kiumbe kimoja kinachofanana na Mwana wa Mutu. Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu inayofika hata kwenye miguu yake na mukaba wa zahabu katika kifua chake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na kati kati ya vile vinara nikaona mtu kwa mfano wa Mwana Adamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.