Revelation 1:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
miguu yake kama shaba iliyong'arishwa iliyosafishwa katika tanuri ya moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya poromoko la maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyayo zake zilikuwa kama shaba inayong’aa katika tanuru la moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mngurumo wa maji mengi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Miguu yake ilikuwa kama shaba ing'aayo inapochomwa katika tanuru. Sauti yake ilikuwa kama kelele za mafuriko ya maji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
miguu yake iling'aa kama shaba iliyosafishwa katika tanuru ya moto na kusuguliwa, na sauti yake ilikuwa, kama sauti ya poromoko la maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
miguu yake kama shaba iliyong'arishwa iliyosafishwa katika tanuri ya moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya poromoko la maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama vile imesafishwa katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyayo zake zilikuwa kama shaba inayong’aa, katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mugurumo ya maji mengi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuri; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
miguu yake kama shaba iliyong'arishwa iliyosafishwa katika tanuri ya moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya poromoko la maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miguu yake ilifanana na shaba nyekundu imulikayo motoni mwa jikoni, sauti yake ilikuwa kama uvumi wa maji mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Miguu yake ilingaa kama shaba iliyosafishwa vizuri sana katika furu ya moto, na sauti yake ilinguruma kama maporomoko ya maji mengi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.