Revelation 1:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua liking’aa kwa nguvu zake zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwa ameshikilia nyota saba katika mkono wake wa kulia. Upanga wenye makali kuwili ulitoka kinywani mwake. Uso wake ulikuwa jua linalong'aa sana mchana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika mkono wake wa kulia, alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mkono wake wa kuume alishikilia nyota saba na kinywani mwake ulitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake kama jua kali linalong'aa kwa nguvu zake zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mkono wake wa kuume alishika nyota saba, na kinywani mwake ulitoka upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa kama jua liking’aa kwa nguvu zake zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aa kama jua kali kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo mkononi mwake mwa kuume alishika nyota saba, namo kinywani mwake mlitoka upanga mkali ulio na makali pande mbili. Nao uso wake ulikuwa kama jua, liking'aa kwa nguvu zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alikuwa ameshika nyota saba katika mukono wake wa kuume. Ndani ya kinywa chake mulitoka upanga wenye makali ngambo zote mbili, uso wake ulingaa sana kama jua wakati linapopiga vikali sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.