Revelation 1:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siri ya nyota zile saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia na siri ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu, ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa makanisa; na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni makanisa saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makundi saba ya waumini, navyo vile vinara saba ni hayo makundi saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ni maana iliyofichwa ya nyota na vinara saba vya taa vya dhahabu ulivyoviona: Vinara saba ni makanisa saba. Nyota saba ni malaika wa makanisa saba.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siri ya nyota zile saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia, na siri ya vile vinara saba vya taa hii: zile nyota saba ni malaika wa makanisa; na vile vinara saba vya taa ni makanisa saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siri ya nyota zile saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia na siri ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu, ni hii: zile nyota saba ni malaika wa makanisa; na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni makanisa saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, navyo vile vinara saba ni hayo makanisa saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makundi saba ya waumini, navyo vile vinara saba ni hayo makundi saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siri ya nyota zile saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia na siri ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu, ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa makanisa; na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni makanisa saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Liandike fumbo la zile nyota saba, ulizoziona mkononi mwangu mwa kuume, nalo fumbo la zile taa saba za dhahabu. Zile nyota saba ndio malaika wa makundi saba ya wateule, nazo taa saba ndio makundi saba ya wateule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ndiyo maana ya lile fumbo juu ya zile nyota saba ulizoona katika mukono wangu wa kuume, na vile vinara saba vya zahabu: zile nyota saba ni wamalaika wa makanisa saba na vile vinara saba ni yale makanisa saba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.