Revelation 1:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Heri yake mtu anayesoma kitabu hiki chenye maneno ya ujumbe wa kinabii; na heri yao wanaosikia na kushika yaliyoandikwa humu, maana wakati wa mambo haya umekaribia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ana heri anayesoma maneno ya ujumbe huu kutoka kwa Mungu kwa kupaza sauti na wale wanaousikia ujumbe huu na kuyatendea kazi yaliyoandikwa ndani yake. Wakati uliosalia ni mfupi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Heri yake mtu anayesoma kitabu hiki; heri yao wale wanaosikiliza maneno ya ujumbe huu wa kinabii na kushika yaliyoandikwa humu, maana wakati umekaribia ambapo mambo haya yatatukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Heri yake mtu anayesoma kitabu hiki chenye maneno ya ujumbe wa kinabii; na heri yao wanaosikia na kushika yaliyoandikwa humu, maana wakati wa mambo haya umekaribia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na pia wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu, na wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati uko karibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Heri yake mtu anayesoma kitabu hiki chenye maneno ya ujumbe wa kinabii; na heri yao wanaosikia na kushika yaliyoandikwa humu, maana wakati wa mambo haya umekaribia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenye shangwe ndio wanaoyasoma nao wanaoyasikia maneno ya ufumbuo huu na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwani siku ziko karibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Heri yule anayesoma na wale wanaosikia maneno hayo ya unabii na kushika yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki, kwa maana wakati wa kutimia kwa mambo haya unakaribia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.