Revelation 1:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Yohane nayaandikia makanisa saba yaliyoko Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yohana. Kwa makundi saba ya waumini yaliyo jimbo la Asia. Neema na amani ziwe kwenu kutoka kwake aliyeko, aliyekuwako, na atakayekuja, na kutoka kwa wale roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kutoka kwa Yohana, Kwenda kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema na amani ziwe kwenu kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo daima na anayekuja; na kutoka katika roho saba zilizoko mbele ya kiti chake cha enzi;
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi Yohane nayaandikia makanisa yaliyoko mkoani Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Yohane nayaandikia makanisa saba yaliyoko Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja na kutoka kwa wale Roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yohana, kwa makundi saba ya waumini yaliyoko Asia: Neema na amani iwe kwenu kutoka kwake aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, na kutoka kwa wale roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Yohane nayaandikia makanisa saba yaliyoko Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Yohana nawasalimu ninyi makundi saba ya wateule yaliyoko Asia. Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwake yeye aliopo, aliyekuwapo, atakayekuja! Tena unatoka nako kwao roho saba walioko mbele ya kiti chake cha kifalme,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mimi Yoane ninayewaandikia ninyi makanisa saba munaokuwa katika jimbo la Azia. Ninawatakia neema na amani kutoka kwa Mungu anayekuwa, aliyekuwa na anayekuja, na kutoka kwa roho saba wanaokuwa mbele ya kiti chake cha kifalme,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi: