Revelation 1:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tazama! Anakuja na mawingu,” na “kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma”; na makabila yote duniani “yataomboleza kwa sababu yake.” Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tazama, Yesu anakuja pamoja na mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma. Watu wote wa dunia watamwombolezea. Ndiyo, hili litatokea! Amina.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tazama! Anakuja katika mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama! Anakuja na mawingu na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma mkuki; na mataifa yote ulimwenguni yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama! Anakuja na mawingu, na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma; na makabila yote duniani yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na makabila yote ya dunia yataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama! Anakuja na mawingu! Kila mtu atamwona, na hata wale waliomtoboa. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, anakuja mawinguni, macho yote yatamwona, nayo yao waliomchoma; ndipo, makabila yote ya nchini yatakapomlilia. Ndio, ni kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia, yeye anakuja katikati ya mawingu! Kila mutu atamwona, hata wale waliomutoboa kwa mukuki. Na kwa sababu yake mataifa yote ya dunia yatalalamika kwa huzuni. Hakika ni vile! Amina.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.